Mapenzi ni kitu Fulani tofauti sana
kwenye hii dunia na hata nje ya hii sayari. Mapenzi kwa kiasi kikubwa sana
yanasababisha hata mambo mengine kwenye hii dunia yaende sawa au yaende tofauti
hata kama hayahusiani na mahusiano ya mapenzi. Vifo vingi hutokana na mapenzi,
kuna magonjwa watu wanaumwa kisa mapenzi, kuna mambo watu wanayafanya si ya
kawaida kisa mapenzi.
Ukiachilia mbali PESA, Mapenzi huwa yana
nafasi kubwa sana kwenye kitu chochote ndani yahii dunia tunayoishi. Si
masikini wala si tajiri, wote kwa pamoja wanahitaji mapenzi kutoka kwa wanaowapenda
ili dunia iweze kwenda sawa kwa upande wao. Na ndio sababu hata mimi hapa
ninaandika kuhusu mapenzi kwa sababu yananigusa hata mimi na hata wewe
unayesoma hapa sasa.
Ukipata mpenzi anayekuelewa na kukupenda
basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako utaiona inazunguka kama kawaida na
maisha yatasonga mbele kwako kwa raha mustarehe, na hata matatizo mengine
makubwa kwako huwa madogo kwa sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.
Lakini ukiumizwa kwenye mapenzi au
kutojaliwa kama wewe unavyojali basi hata dunia iwe na raha gani kwako utaiona
chungu na hata raha ya maisha hutakuwa nayo hata kama una hela kiasi gani na
hata kama una cheo kikubwa kama mfalme au hata rais. Wengine hufikia hatu ya
kuteseka tu bila kuondoka kwenye mahusiano kwa kuogopa kuumizwa tena huko
waendapo na wengine huondoka baadae sana wakiwa tayari wameshachelewa.
Kuna Sababu Nyingi Sana zinazoweza
kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata
kusababisha kuachana. Mojawapo kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi
zifuatazo;-
1. UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye
mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa
sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa
wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni
muongo/anamdanganya.
Kuna vitu vingine hata kudanganyana
haileti maana wala haina tija kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote
lile ni jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua
unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.
2. USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni
pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye
mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana
na mapenzi yenu moja kwa moja. Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa
sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni
lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.
Kama kuna kitu hukuwahi kumwambia na unahisi
ukimwambia atakasirika ni bora umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko aje
kugundua mwenyewe itakuwa shida sana kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye mahusiano
mwaka wa 4 sasa na kumbe kabla ya kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una
watoto 2 kwa huyo mke/mume wa mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza
kukuelewa lakini mara nyingi ni kwa shingo upande.
3. ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye love kama kugundua kuwa
Yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana
mtu mwingine zaidi ya wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha
hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa bado wanapenda
pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye mapenzi.
Kamwe Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye
Ajutie Penzi Lako, Usimfanye Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni
Ujanja Lakini Ipo Siku Utahitaji Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata,
Laana Ya Mapenzi Ipo, Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi Ya
Kweli Yanawezekana Kama Ukiamua na si kwa ku-cheat.
4. DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza
mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda
mtu wako kwa khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au
ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe
nani.
Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati
ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri au hata
akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya
wapenzi wao kiuwezo, ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa Linapokuja
Suala La Ndoa/Kuishi Na Mtu, Kwetu Sie Wanaume Huwa Hatuangalii Uzuri/Urembo Wa
Mwanamke Kama Ndio Kigezo Pekee Cha Kufanya Tumuoe/Tuishi Na Huyo Mwanamke,
Ingekuwa Hivyo Basi Wanawake Wote Warembo/Wazuri Wangekuwa Ndani Ya Ndoa Leo
Hii, Hii Inamaanisha Kuwa Hata Ukiwa Mrembo/Mzuri Hutakiwi Kujisahau Ukaona
Umeshafika...Utapotea ukileta dharau kwa uzuri wako au uwezo ulionao.
5. MROPOKAJI/ASIYE MSIRI.
Hakuna kitu kinachoweza kumfanya mwenza wako
kukukimbia au hata kukosa uaminifu na wewe kama akija kugundua kama wewe ni
mropokaji na huna ‘’kifua’’ hasa kwa yale mambo ambayo ni ya chumbani na
hayakutakiwa kutoka nje. Hakuna mtu anayependa siri zake kutoka hadharani na
huwa inaumiza sana kwenye mapenzi kumpa mtu siri zako then yeye anaenda
kusimulia.
Mambo mnayafanya mkiwa wawili tena ndani lakini
kesho unaenda mtaani unakuta kila mtu anajua mlichofanya tena wanakuhadithia
kama walikuwepo vile, hiyo si kitu nzuri na itakufanya ukimbiwe na kila mpenzi
unayempata.
6. TAMAA/KUKOSA UVUMILIVU.
Tamaa ni kitu kingine ambacho hufanya mahusiano
mengi kukosa nguvu na mengine kuvurugika kabisa. Kama mpo kwenye mapenzi na
mmeamua kupendana kwa shida na raha basi haitakiwi mmoja wenu kuwa na tama na
kukosa uvumilivu hata kwa yale mambo yanayoweza kuzuilika.
Kama mpenzi wako ni wa hali Fulani na umeamua kuwa
naye basi usiwe na tama kwa vitu vingine ambavyo vinaweza kukusababishia
mahusiano yako kukosa nguvu na kufa kabisa. Amini kuwa ipo siku mtakuwa na vitu
kama unavyotamani kwa kuongeza bidii kutafuta na kushauriana nini cha kufanya
lakini si kwa kutafuta ‘’shotcut’’/njia nyepesi nyepesi zinazoweza kuku-cost
hapo baadae.
7. KUKOSA MSIMAMO.
Hii kitu huwakuta wengi sana kwenye mapenzi ya siku
hizi. Nadhani ni hali halisi ya dunia ya sasa inachangia pia pamoja na
teknolojia tuliyonayo ya kutuwezesha kufanya yale tunayoyaona kwenye mitandao
na vyombo mbali mbali vya habari.
Wapenzi wengi siku hizi wamekosa msimamo kwenye
mapenzi/mahusiano yao na unakuta tu mmoja anakuwa na wapenzi zaidi ya mmoja na
wanakuwa hawafahamiani huku kila mmoja akijua kuwa yeye ndo kila kitu kwa
mpenzi wake.
8. KUTOJALI/KUTOKUWA NA MSAADA.
Hii pia kwa kiasi kikubwa inaumiza sana na kupelekea
kushuka kwa thamani ya mapenzi miongoni mwa mahusiano mengi haa duniani. Kama
kweli unampenda mpenzi wako basi msaidie anapopata matatizo na umjali na
kumchukulia kama mpenzi wako na mtu wako wa karibu na sio kukimbia majukumu
bila sababu zote za msingi.
Kama huwezi kujali na kusaidia basi usiingie kwenye
mahusiano ni bora ukae mwenyewe kuliko kuwepo sehemu usiyotakiwa.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.