Siku zote hatutaacha kuzungumza juu ya mapenzi kwani ni ukweli usiopingika kwamba, nyanja hii imechukua nafasi kubwa katika maisha yetu.
Tunafanya kazi usiku na mchana, tunahangaika huku na huko lakini mwishowe tunafikiria jinsi ya kuboresha na kufurahia maisha na wapenzi wetu na kupata utulivu na amani katika maisha ya kimapenzi.
Ndiyo maana kila mmoja anajitahidi kutafuta mwenza sahihi ambaye anaweza kumfanya asijute kuwa naye na mwishowe furaha itawale.
Lakini katika jamii yetu kuna watu ambao kutokana na ugumu wa maisha ama tamaa zao wameamua kuigeuza miili yao kuwa kitega uchumi. Wanawake hawa wako tayari kulala na mwanaume yoyote ili mradi wapewe fedha.
Kwa kifupi watu hawa wanadharauliwa na kila mmoja atashangaa kuona au kusikia mwanaume anaoa msichana aliyekuwa malaya. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, kuna wanaume wanawaoa. Katika hili hata wewe unaweza kuwa shahidi.
Kuna wasichana huko mtaani wanajulikana kuwa ni machangu lakini siku ya siku unasikia mmoja wao kaolewa. Mbaya zaidi anaolewa msichana wa sampuli hiyo anaachwa msichana aliyetulia.
Katika kupekuapekua nimebaini sababu tatu ambazo zinawafanya baadhi ya wanaume wawaache wasichana waliotulia wenye uzuri wa sura, tabia na maumbile na kwenda kuwaoa wasichana micharuko.
Wanabadilishika
Uchunguzi unaonesha kuwa, asilimia kubwa ya wasichana ambao walikuwa wakijiuza waliopata wanaume wa kuwaoa, wamebadilika na kuwa wake wema kwa waume zao.
Inakuwa hivyo kwa kuwa wanaochukulia ile kuolewa kama bahati hasa kwa wale ambao walikuwa wakijiuza kutokana na ugumu wa maisha.
Wanatulia wakijua wana uhakika wa kuishi na hivyo wanajiona wana kila sababu ya kuwapenda, kuwaheshimu na kuwanyenyekea wanaume walioacha wasichana waliotulia majumbani kwao na kuwaoa wao.
Wanayajua ‘majambozi’
Hili halina ubishi, wanawake wengi ambao wamebobea kwenye umalaya ni wazoefu. Asilimia kubwa ni watundu na wabunifu wanaojua mbinu za kuwatuliza na kuwadatisha wanaume. Kwa kuwa wanaume wanapenda wanawake wanaoyajua ‘majambozi’, baadhi yao wanaona ni bora kuwaoa hao wakiamini wakipatilizwa watatulia.
Katika upekupeku wangu nimebaini pia wapo wasichana waliokuwa wakijiuza maeneo maarufu ya jijini Dar lakini leo hii ni wake za watu waliotulia na wanaziheshimu ndoa zao.
Wakiolewa hawadanganyiki
Baadhi ya wanaume wanaeleza kuwa, ni bora kuoa msichana wa mjini ambaye ameshafanya kila aina ya ufuska kisha akatulia kuliko kumuoa msichana kutoka kijijini ambaye hajui chochote.
Wanaeleza kuwa, msichana aliyetulia akija kuolewa kisha akajanjaruka, raha ya ndoa inaweza kutoweka (si wote waliotulia wakiolewa wanajanjaruka na kuanza vituko).
Lakini pia mwanamke ambaye alikuwa malaya hawezi kudanganyika kirahisi kwa wanaume. Ameshakutana nao wa kila aina, warefu na wafupi, waongo na wakweli hivyo anaona ni bora kumuamini yule mmoja aliyemuweka ndani tu.
Hizo ndizo sababu tatu za baadhi ya wanaume kupenda kuoa malaya. Hata hivyo, ukweli unabaki kuwa, mwanamke anatakiwa kujituliza. Kujiuza ni haramu na kujidhalilisha. Wale waliokuwa malaya kisha wakaolewa waone ni bahati kwao lakini malaya hana nafasi kwa mwanaume.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.