Featured Posts

BAADA PICHA ZAO ZA KIMAHABA KUVUJA MTANDAONI,SNURA AFUNGUKA KIIVI...!SHUKA NAYO HAPA..!

Baaada ya Staa wa sinema na muziki Bongo, Snura Anton Mushi na Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa kunaswa kimahaba hapo jana, leo Mwanadada Snura Mushi amfunguka na kudai kuwa Ngassa ni rafiki yake tuu na si vinginevyo.
 Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi na Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo zangu.Ngassa alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani kwangu. Simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli ndiyo huo.”

Kwa upande wake Ngassa ambaye yupo mapumzikoni baada ya kumalizika kwa msimu wa kwanza wa Ligi Kuu Bara hakuweza kusema chochote kufuatia simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.  

Hapo awali ilidaiwa kuwa wawili hao walibambwa wakiwa wamejiachia ‘wakifanya yao’.
Mnyetishaji huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa wakiminyana bila kujali macho ya watu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Snura hasa marafiki na majirani zake.“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila kificho chochote.
 

Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.  “Baadaye hata Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku akicheza na nywele za Snura anavyotaka,” alidai shuhuda wetu.  

Ili kujiridhisha, Tulisaka picha za wawili hao ambazo walikuwa ‘wakijifotoa’ kwa simu zikiwaonesha wakiwa katika mahaba jambo lililozua utata na maswali kwa walioziona.

Uchunguzi ulibainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa Snura na Ngassa kunaswa wakiwa beneti kwani wiki mbili zilizopita walibambwa kwenye ukumbi mmoja wa starehe jijini Dar wakila bata ndefu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.